const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Tz Town Tv: WADAU WALALAMIKA KUTO KUWAPO KWA DAWA LICHA YA KUUNGANISHWA - HABARI MPYA

..

Tz Town Tv: WADAU WALALAMIKA KUTO KUWAPO KWA DAWA LICHA YA KUUNGANISHWA

WATOA huduma wa mfuko wa bima ya afya taifa NHIF mkoani Njombe wamemuomba Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo Anne Makinda ambaye pia ni spika mstaafu kuwasaidia kupata malipo yao kwa wakati ili waweze kununua madawa na vifaa tiba na kuboresha kwa wananchama wake.

Ombi hilo kwa mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo wakati wa mkutoano na watumishi wa mfuko huo pamoja na wadau mbalimbali mfuko huo mkoani Njombe ambapo watoa huduma za afya wakionywa kauli mbaya kwa kwa wateja wao.

Watoa huduma za afya wanao shirikiana na mfuko huo pamoja na wateja wake wamelalamikia kuwapo kwa uchelewashwaji wa pesa za wateja walio hudumiwa na wengine wakisema kuwa vituo vya afya vya serikali kukosa dawa ni kero.

Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Makinda anasema kuwa mfuko huo sasa umedhamilia kuhakikisha kuwa wateja wake wanaona raha kuwa wanachama kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.
Makinda anasema kuwa haiwezekani mtu anaumwa akapokelewa kwa matusi na maneo makali ambayo yanaongeza maumivu kwa wagongwa  licha ya kuwa amejiunga na huduma za bima ya afya.
“Haiwezekani mtu akawa amejiunga na mfuko wa bima ya afya akitegemea huduma ya afya baada ya kulipia lakini anapokelewa na maneno makali unafikili mgonjwa huyo atapona kweli maana hata dawa anakuwa na wasiwasi nazo, kwani wewe mhudumu unanufaika na nini unapotoa maneno hayo,” alisema Makinda.

Mmoja wa maafisa wa mfuko huo mkoani Njombe, Juma Michael ambaye ni afisa matekelezo anaeleza changamoto zinazo wakabili wakati wa kutoa huduma kwa jamii ambapo ni baadhi ya vituo wahudumu wake kuw ana kauli mbaya kwa wateja.

Mfuko wa bima ya afya NHIF hadi kufikia mwezi Desemba mwaka 2016 umeweza kusajili wananchama  6998 sawa na asilimia 80 ambapo lengo ni kufikia asilimia 85 hadi kufikia mwaka 2020.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI ......................



Mvua Mwisho April tazana itakavyo katika..............


Related Posts

Post a Comment