WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya muungano Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Njombe Kuunda tume ya siku moja kuchunguza suala la bili za maji na mfumo uliotumika kupandisha bili za maji mjini hapo na baada ya hapo serikali itatoa maamuzi.
Agizo hilo linatolewa katika mkutano wa hadhara ambapo mbunge
wa Njombe Mjini Mhe. Edward Mwalongo ambaye ametoa malalamiko ya wananchi mbele
ya waziri Mkuu ambapo serikali inasema kuwa imeandaa fedha kwaajili ya
kumamilisha miradi mbalimbali.
Ni mabango ambayo yanaambatana na kerere za shangwe ambazo zinampokea
huku nyimbo nazozikichagiza.
Mbunge anasimama mbele ya kipaza na kuwasemea wananchi ambapo
miradi ya maji ikitawala maombi yake na kusema kuwa kuna miradi mikubwa
inasuasua.
Waziri Mkuu anaanza na bili za maji kwa kumuita mkurugenzi wa
Maji halmashauri ya Mji Njombe Daudi Majani kuelezwa wananchi ambapo anabaini
madudu.
Hata hivyo waziri mkuu anatoa agizo kwa mkuu wa mkoa wa
Njombe kuhusu masuara kupanda kwa bei ya maji na matumizi ya fedha za maji
zinazo kusanywa.
Masuala mengine yaliyo ibuka katika mkutano wake ni pamoja na
ardhi barabara na huduma za Afya ambapo serikali inaekezwa kuwa imetwenga
Bilioni 200 kwaajili ya dawa pekee na zimekabishiwa kwa bohari ya dawa MSD na
kuwa malengo ya serikali ni kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana kula pahala
palipo na wananchi.
Waziri mkuu kabla ya kukutana na wananchi wa mji wa Njombe
anatembelea stendi ya mabasi ya mkoani Njombe inayo jengwa kwa thamani ya zaidi
ya shilingi bilini 9 za kitanzania lakini kauli ya serikali akiwa hapa
inatolewa na mkuu wa mkoa kuachiwa jukumu huku ziara yake ikihitimishwa mkoani
Njombe anakutana na watumishi wa serikali.
TAZAMA VIDEO HAPA WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WAKAZI WA NJOMBE NI KUHUSU MAJI, AFYA
Post a Comment
Post a Comment