WAFANYABIASHARA hapa nchini wameiomba serikali kuboresha mtandao wa mashine za kukusanyia mapato katika vizuizi mbalimbali vya kukusanya mapato ili kuendana na muda na kuwapunguzia gharama.
Kutokana na matatizo ya mtandao wa mashine za kukusanyia ushuru katika vizuizi mbalimbali vya halmashauri, baadhi ya wafanyabiashara wamesema wamekuwa wakilala polini.
Jambo hili linafika katika baraza la madiwani halmashauri ya Mji Makambako ambapo madiwani wanaomba halmashauri kutatua kero hiyo.
Kero hiyo pia inawatesha hata watendaji katika kukamilisha kazi zao na kusababisha kuwachelewesha wateja wao.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji huo Paulo Malala anasema kuwa serikali inaendelea kuboresha mtandao.
TAZAMA EFD ZINAVYO CHEREWESHA WAFANYABIASHARA MPAKA KULALA PORINI
Post a Comment
Post a Comment