UTAFITI unaonyesha kuwa ni asilimia saba pekee kwa mkoa wa halmashauri ya Njombe hospitali zinatumia maji yaliyo tibiwa na kusababisha watoa huduma wa afya kusambaza magonjwa kwa wagonjwa kutokana na maji yasiyo salama.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti wa majenjwo ya binadamu ya taifa Nimr uliofanywa kwa wilaya nane hapa nchini unatolewa wilayani Njombe na kubainisha haya.
Mtafiti kutoka Nimr Dr. Hamis Marebo anasema kuwa kutonawa vizuri mikono kunaweza sababisha magonjwa kwa mtu haijarishi ni wapi na kuwa magonjwa mengi watu wamekuwa waklipata magonjwa wakiwa Hospitali.
Kutokana na utafiti huo Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe anasema kuwa sasa wanaenda kujipanga kuondoa changamoto zinazoweza kuzuirika.
Wahandisi, maafisa wa afya, wakuu wa vituo vya afya na maafisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya Njombe wanapatiwa utafiti huu na kutaja vitu wanavyo kwenda kuvifanya.
Post a Comment
Post a Comment