TAASISI ya Internet Society Tanzania (ISOC), ambayo ni tawi la Taasisi ya Internet Foundation ya nchini Marekani, imewataka watanzania kuhakikisha wanatumia mfumo mtandao wa Encryption ambao utawasaidia kutunza siri za taarifa zao katika mtandao wa internet kuingiliwa na wahalifu.
Hayo yameelezwa na Rais ISOC Nazar Kilama, katika mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo huo wa Encryption yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, yakiwa yameandaliwa na a taasisi hiyo kwa kushirikiana na Organisation of Digital Africa (ODA).
Kilama, amesema mfumo wa Encryption hufanya taarifa zote za mtumiaji wa mtandao wa internet kuwa salama, bila kuingiliwa na mtu yoyote hivyo kuwa na uhakika wa mawasiliano salama.
Kilama ameeleza, watumiaji wa internet wanaweza kutumia mfumo huo kwa kuupakua na kuhifadhi katika simu zao za mikononi au kompyuta na taarifa zao hazitaweza kuingiliwa na mtu yoyote nje ya mfumo tofauti na sasa ambapo taarifa nyingi za mawasiliano ya internet huweza kuhujumiwa.
“Ukiwa na Encryption katika kompyuta au simu taarifa zako zitakuwa ni salama labda zivujishwe na mtu mwingine uliyewasiliana naye. Pia mfumo huu ni usalama kwa mtu binafsi, taasisi za umma, binafsi na serikali,”ameeleza.
Post a Comment
Post a Comment