const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Iringa waungana na Rais Samia kuwafariji wananchi wa Hanang' - HABARI MPYA

..

Iringa waungana na Rais Samia kuwafariji wananchi wa Hanang'


Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Mhe. Halima Omari Dendego, amekabidhi  misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40  kutoka kwa wafanyabiashara mkoani humo na ofisi yake kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.

Dendego amesema wameguswa na tukio hilo na kuamua kumuunga mkono Rais Samia katika kutoa faraja huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kuungana na serikali katika kipindi hiki kigumu wanachopitia wananchi hao wa Hanang' .

Ametaja misaada waliyoitoa ni chumvi pakiti 1,  mahindi gunia 1, ndoo ndogo 100, mashuka duvet matatu, unga viroba vya kilo tano 100, magodoro 3x6  20, mchele viroba vya kilo 25 120, unga viroba vya kilo 25  200,mkaa mweupe gunia 350 na Milunda ya miti, miti 8000 itakayosaidia kwenye ujenzi wa nyumba za muda, ambavyo vyote gharama yake ni shilingi milioni 42,944,000.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo katika shule ya msingi Katesh, Mkuu wa wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja amewashukuru wafanyabiashara na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa  kwa kujitoa kwao kumuunga mkono Rais Samia katika kusaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya QWIHAYA Ndugu Leonard Mahenda ambaye ametoa Milunda ya miti 80,00, amesema miti hiyo itakwenda kuzisaidia zile kaya zisizo na nakazi wakati serikali ikiendelea na jitihada za kuwajengea nyumba zaingine.

Kwa sasa shughuli mbalimbali zimeanza kurejea taratibu  katika mji mdogo wa  Katesh na kata zingine zilizoathirika na maafa hayo makubwa yalioacha Simanzi na majonzi.

Related Posts

Post a Comment