const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Benki ya NMB kupitia Reliance Insurance yatoa fidia kwa wafanyabiashara Hanang'. - HABARI MPYA

..

Benki ya NMB kupitia Reliance Insurance yatoa fidia kwa wafanyabiashara Hanang'.


Na John Walter-Manyara

Benki ya NMB kupitia Kampuni ya Reliance Insurance, imewalipa fidia ya Shilingi Milioni 269,673,837 wafanyabiashara 18 waliokata bima mbalimbali, kati ya waliokumbwa na maafa ya maporomoko ya tope,mawe na magogo wilayani Hanang Disemba 3,2023.

Hafla ya kuwakabidhi wafanyabiashara hao hundi yenye thamani hiyo, imefanyika Januari 11,2024 katika eneo la stendi ya mabasi Katesh, ambako wahanga hao wamekiri kuwa hasara na maumivu yao ya kuharibiwa kwa biashara zao yamepozwa na malipo hayo ya bima.

Mkuu wa Kitengo cha Bima Benki ya NMB, Martin Massawe, ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujilinda kwa bima mali na pesa wanazotafuta kwa jasho ili kuepuka maumivu yasiyo na mfariji yanapotokea majanga.

Massawe amesema janga la Hanang' liwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine kuona umuhimu wa kukata bima,kwani siku zote majanga huja bila kutarajia na kwamba BIMA inalipa.

Hata hivyo benki ya NMB imeahidi kuendelea kutoa elimu kwa watu wote juu ya umuhimu wa kukata Bima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, amesema ni takwa la kisheria kwa mtu yeyote aliyekata bima ya majanga katika biashara yake, nyumba, gari, mashamba na zingine kupewa haki yake pindi majanga yanapotokea.

Aidha  Dkt. Saqware amewapongeza waathiriwa hao kwa uamuzi wao wa kukata bima, huku akisisitiza wengine kuwa na utaratibu huo ili kujisaidia wenyewe wakati wa matatizo au majanga yanapotokea.

Akisisitiza umuhimu na unafuu wa bima hizo, Dkt. Saqware amesema Uwepo wa bima hurejesha nguvu haraka kwa muathirika pindi janga linapotokea huku akitoa wito kwa wafanyabiashara na watu wengine kukata Bima mbalimbali kwa ajili ya kujiwekea kesho nzuri kwani hakuna ajuaye muda wa majanga kutokea.

Mwakilishi wa Kampuni ya Reliance Insurance, Cornel Joachim  amesema ni muhimu kila mmoja akawa na Bima kwa kuwa majanga hayabishi hodi na bima hizo sio kwa biashara tu bali zipo za magari,nyumba,moto na nyingine nyingi na kwa sasa wanazo hadi bima za wajasiariamali wadogo kama machinga na boda boda.

Mkuu wa wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja, amesema wafanyabiashara waliopatwa na janga hilo ni wengi lakini 18 pekee ndio waliokata Bima, hivyo ni fursa kwa wengine kuona umuhimu wa kukata Bima kwenye biashara zao.

Mayanja meziomba  Benki zote ziwe na dirisha maalum la kuendelea kuwajengea uwezo na kuwasaidia wafanyabiashara walioathiriwa na mafuriko hayo ya Hanang' waweze kujipanga na kurudi katika utafutaji na kuchangia pato cha nchi.

Related Posts

Post a Comment