const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Shilingi bilioni 2.36 kutumika kwa miradi miwili ya maji ya Nanguru Corridor na Mkwajuni- Nanjime. - HABARI MPYA

..

Shilingi bilioni 2.36 kutumika kwa miradi miwili ya maji ya Nanguru Corridor na Mkwajuni- Nanjime.

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.


Serikali inatarajia kutumia shilingi 2,369,121,784.34 kugharamia miradi  ya maji ya Nangaru Corridor na Mkwajuni- Nanjime ambayo ipo katika wilaya ya Lindi.


Hayo yameelezwa leo na kaimu meneja wa wilaya ya Lindi wa Wakala wa Usambazi Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(Rural Water Supply and Sanitation Agency/ RUWASA), mhandisi Nassoro Mohamed  kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Mkwajuni na Nangaru wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi maeneo ya miradi hiyo.


Mhandisi Nassoro alisema mradi wa Mkwajuni Nanjime ambao utawanufaisha wananchi 3,045 waliopo katika vijiji vya Nanjime na Mkwajuni  utagharimu shilingi bilioni 1,052,706,349.34. Ambapo mradi wa Nangaru Corridor ambao utawanufaisha wananchi 5,904 waliopo katika vijiji vya Uleka, Muungano na Mkumbamosi utagharimu shilingi 1,316,415,334. 


Alisema miradi hiyo itatekelezwa kwa awamu mbili. Ambapo fedha hizo zitatumika katika awamu ya kwanza na kuwanufaisha wakazi hao 8,949 waliopo katika vijiji hivyo vya Nangaru Uleka, Muungano, Mkumbamosi, Nanjime na Mkwajuni.


" Katika awamu ya pili ambayo  itaanza kutekelezwa kwa kutumia fedha za bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025 itawanufaisha wananchi waliopo katika vijiji vya Kingulungundwa, Kiwalawala, Mjimwema, Kitomanga, Makumba, Komolo na Kipunga," alisema mhandisi Nassoro.


Kaimu meneja huyo alizitaja  kazi zitakazo fanywa na mkandarasi huyo, kampuni ya scorpion kuwa ni matangi ya kuhifadhia maji, ujenzi wa mabomba makuu na mitandao ya maji, ujenzi wa nyumba za mitambo na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji.


Alizitaja kazi nyingine kuwa ni uwekaji wa mfumo wa umeme na ufungaji wa mambo wa kuvuta maji. Huku akibainisha kwamba muda wa utekelezaji wa miradi hiyo ni siku 180 baada ya wiki mbili tangu siku ya makabidhiano.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alimtaka mkandarasi huyo amalize na kukabidhi kazi hizo kwa wakati kwa mujibu wa mikataba. Huku akimtaka ajenge kwa viwango vilivyopo kwenye mikataba.


Ndemanga pia aliwataka wananchi ambao miradi hiyo inatekelezwa katika vijiji vyao washiriki kikamilifu kufanikisha miradi hiyo. Ikiwamo kuhakikisha wanalinda vifaa vya ujenzi na kumsaidia mkandarasi katika eneo la nguvu kazi. Hasa vibarua.


Related Posts

Post a Comment