KAMATI za afya za mitaa ya kata tatu za Halmashauri ya Mji Njombe zimepatiwa elimu juu ya majukumu yao, Mipaka na kazi ambazo wanatakiwa kuisaidia huduma ya za afya huku kamati hizo zikitakiwa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitatu na si vinginevyo.
Elimu hiyo inatolewa ili kuboresha huduma za afya katika ngazi za mitaa na kusimamia watoa huduma wanaotoa Mbovu na matusi kwa wateja wao huku wakiagizwa kwenda kusimamia uhamasishaji wa kujiunga na mifuko ya afya ya jamii.
Shirika lisilo la kiserikali la Highlands Hope Umbrella ya mjini Njombe inatoa elimu hii kwa kamati ya afya kwa kata tatu za Mji Mwema, Njombe Mjini na Ramadhani ambapo kila mtaa wajume wajumbe watatu wamepatiwa elimu hiyo.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja diwani wa Kata ya Njombe mjini anasema ni muhimu wanao jifunza wakawa makini ili kamati hizo zikafanya kaziyake ipasavyo.
Wakufunzi wanasema kuwa wanakamati hao wanamipaka yao na kuwa uwezo wa kupanga bajeti ya afya kwa zahanati zao.
Wanao jifunza wanasema kuwa sasa wanaenda kuwaelimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko ya afya na kufahamisha uma mahala pa kupeleka malalamiko yao.
Jamii kubwa bado haifahamu majukumu ya kamati za afya za mitaa na vijiji huku ukomo wake na kamati nyingi kuto jua majukumu yake na ukomo wake.
Post a Comment
Post a Comment