const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); TzTown Tv: Viazi Kutoka nje ya nchi vyaharibu soko la Bongo - HABARI MPYA

..

TzTown Tv: Viazi Kutoka nje ya nchi vyaharibu soko la Bongo

Post a Comment
Wakulima wa viazi mviringo mkoani Njombe wameiomba serikali kudhibiti uingizwaji wa zao hilo kutoka nchi ya jirani ya Kenya ama kuweka vifungashio vya aina moja ili kuingia katika soko la viazi na kushindania wateja kwa pamoja vikiwa na ujazo sawa.

Wakulima wa vijiji vya Njomlole na Mfeleke wamesema kuwa viazi vyao sasa havichimbwi kutokana na wafanyabiashara kufika katika maeneo yao na kuwatajia bei ambayo hairejeshi gharama za uzalishaji kwa madai kuwa sokoni kuna viazi kutoka nchini Kenya.

Wakulima wa viazi katika vijiji hivyo wanasema kuwa kwa bei ya shilingi elfu 30 na 20 hawatachimba viazi kutoka katika mashamba yao licha ya kuwa na viazi vipo tayari kwa kuvunwa.
Wamesema kuwa kama viazi vitanunuliwa kwa bei hiyo hawatapata faida hata kidogo na watashindwa kulima katika msimu ujao.

Wameongeza kuwa wafanyabiashara wakifika mashambani wanaangalia viazi na kuwaambia kuwa watanunua kwa bei hiyo kwa sababu serikali inawasumbua barabarani wakielekea Sokoni jijini Dar es salaam na wakifika sokoni pia wanakutana na viazi kutoka nchi ya Kenya.
Diwani wa kata ya Uwemba anaiomba serikali kuwatengeneza mazingira mazuri wakulima ili waweze kuendelea na shughuli za kilimo na kujikwamua na hali duni ya kipato katika familia zao.

Wafanyabiashara wanakiri kuwepo kwa usumbufu barabarani na changamoto nyingine wanapofika sokoni.
Hata hivyo wafanyabiashra wanatoa ushauri kwa serikali kuhusu vifungashio vya viazi.
Aidha wataalamu wanaoshawishi wakulima kulima viazi mviringo kibiashara wamesema wakulima wengi wamekuwa wakilima viazi bila kufuta kanuni hali inayosababisha kuzalisha viazi vinavyoshindwa kuingia kwenye soko la ushindani
Waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara mkoani Njombe amesema kuwa suala la kudhibiti Lumbesa ni suala la kumsaidia mkulima kuuza mazao yake kwa ujazo sahihi.

Wakulima na wafanyabiashara wa viazi mviringo wanashindwa kufikia malengo waliyojiwekea kutokana kutumia vipimo ambavyo sio rasmi ikiwemo visado na Lumbesa
WAKULIMA WALIA NA SOKO LA VIAZI.........................

Related Posts

Post a Comment