MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Njombe imefanikiwa kuzimaleza kesi zake nyingi ndani ya miezi Chini ya 9 na huku zilizozidi muda mrefu ni miezi 12 ambazo zilifunguliwa Mwishoni mwa mwaka jana.
Mikakati ya mahakama ya hakimu mfawidhi Wilaya ya Njombe ni kuhakikisha kuwa haki zinapatikana kwa wakati.
Hayo yanabainishwa wakati mtendaji wa Mahakama, Hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Njombe, na Wakili wa serikali wakizungumzia Utekelezaji wa kazi kwa idara hiyo ya haki.
Mtendaji wa mahakama anasema kuwa kinacho sababisha kesi kuchelewa ni kuwapo kwa mashahidi wanao shindwa kufika mahakamani huku akiwatoa hofu mashahidi kwa kuwa gharama wanazotumia hurudishiwa.
Wakili wa serikali Riziki Matitu anasema kuwa kesi ikifika mahakamani inaruhusiwa Kuondolewa Ila sio ya Jinai.
KUMBE SHAHIDI HULIPWA TAZAMA VIDEO YA UFAFANUZI HAPA......
Post a Comment
Post a Comment