HALMASHAURI ya mji wa Makambako mkoani Njombe imekuli kuwa inauhaba wa magari ya kubebea taka na kusabisha mrundikani wa taka katika baadhi ya visimba vya kukusanyia taka mjini hapo.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo anasema kuwa taka zinakaa katika vizimba hivyo kuanzia siku tatu na zaidi wakati maeneo zikiendelea kutolewa huku wananchi wakilalamikia kuwapo kwa taka hizo pamoja na kulipia pesa za huduma ya uondoaji wa taka hali inayo watia wasiwasi wa kukubwa na magonjwa la mlipuko.
Wananchi mjini humo wanasema kumekuwa na kero kubwa ya kuwapo kwa taka zinazokaa muda mrefu katika vizimba vya taka ambapo huwa kunakuwa na mzalia ya wadudu.
Halmashauri nayo inasema kuwa inakabiliwa na uchache wa magari kitu kinacho sababisha taka hizo kutoondolewa kwa wakati na mara nyingine kuwa na magari mabovu.
Mji wa makambako ni miongoni mwa miji mkoani Njombe inayo kuwa kwa kasi na kuwa na wakazi wengi kitu kinacho sababisha vizimba vya taka kujaa haraka hivyo halmashauri inatakiwa kwendana na ukuaji wa mji huo.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI...........................
Post a Comment
Post a Comment