UONGOZI wa kituo cha kulea watoto yatima cha mtakatifu Anna Uwemba halmashauri ya mji Njombe umeiomba serikali kuwapa leseni ya usajili kwa kuwa taratibu zote za kupata leseni zimekwisha tekelezwa kituoni hapo.
Pamoja lesini kituo hicho inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kuwahudumia watoto hao katika jitihada za kuokoa maisha yao licha ya kutumia gharama kubwa kwenye matibabu.
Wakizungumza mbele ya mbunge wa viti maalumu mkoa wa Njombe Lucia Mlowe wahudumu wa watoto hao yatima ambao ni masister wamesema kituo hicho kimekuwa kikiwalea wataoto wa umri wa chini ya miaka 2 na kwamba kituo hutumia gharama kubwa katika kutoa huduma za afya.
Mara baada ya kuwaona watoto yatima mbunge huyo amesema kituo cha mtakatifu Anna Uwemba ni miongoni mwa vituo vikongwe na kinatakiwa kupatiwa leseni huku akiahidi kufuatilia katika wizara husika.
Mlowe anapita katika kituo hicho ikiwa ni kupita kutoa salamu za mwisho wa mwaka kwa watoto hao na kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto ili wauanze vyema mwaka huu.
Post a Comment
Post a Comment