BAADHI ya wakazi Mkoani Njombe wameitaka serikali kupitia mamlaka ya chakula na dawa TFDA kutoa elimu vijijini na mijini juu ya utambuzi wa bidhaa sisizofaa kwa matumizi pamoja na vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimekuwa vikiiathiri jamii.
Pamoja na elimu, serikali inaombwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini wanaouza bidhaa zisizo salama kwa wananchi huku vijijini ukaguzi uimarishwe na kudhibiti wanao uza bidhaa zilizokwisha muda wake.
Wakazi hawa wanasema licha ya ukaguzi kupita mara kwa mara elimu kwa wakazi wa mjini na vijijini inahitajika ili kutambua bidhaa ambazo zinamadhara kwa matumizi na hatari kwa afya.
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA inatoa elimu kwa wakaguzi wa halmashauri za mkoa wa Njombe ili kupambana na wafanyabiashara wajanja wajanja.
Nini wanaenda kufanya wakaguzi hawa baada ya kupatiwa mafunzo wanasema wataiokoa jamii kubwa na matumizi ya bidhaa feki.
Wakaguzi hawa wanakuwa katika mafunzo ya siku mbili ya kubaini bidhaa ambazo hazijasajiliwa hapa nchini, huku mbinu za kukagua zile zilizo kwisha muda wake wakipatiwa na huku maeneo ya vijijini kukidaiwa kuuzwa zaidi bidhaa zilizokwisha muda wake.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI............
Post a Comment
Post a Comment