CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Njombe kimesema
hakitafanya kazi na mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri kama hataomba radhi ndani
ya siku saba kwa kumuweka ndani mwenyekiti wa mtaa wa Bunguruni Emmanuel
Ngelime tukio ambalo lilitokea Mwishoni mwa mwezi jana mwaka huu.
Chama kimesema kuwa kitendo hicho hakikubaliki na uongozi wa
wilaya hautakubaliana na tukio hilo alilofanyiwa mwenyekiti mwenyekiti wao.
Viongozi wa wilaya, madiwani na wenyeviti wa mitaa kupitia Chadema
wanaketi kikao cha siku tatu cha kutafakari juu ya jambo alilolifanya mkuu wa
wilaya ya Njombe la kumuweka ndani kwa masaa 48 mwenyekiti wa mtaa.
Madiwani kupitia chama hicho wanasema kuwa hawapo tayari
kushirikiana na mkuu hiyo wa wilaya kwa wakipinga kile alicho kifanya kwa
mwenyekiti huo.
Mwenyekiti wa chama hicho wilya ya Njombe Abuu Mtamike ambaye
pia ni diwani wa kata ya Mjimwema anasema kuwa wanatoa tamko la kuto shirikiana
naye katika shughuli yoyote ya kimaendeleo na kuwa wanamtaka aombe msamaha
ndani ya siku saba.
Mkuu wa wilaya ya Njombe mwishoni mwa mwezi jana kwa mujibu
wake alimuweka ndani mwenyekiti huyo kwa madai ya kumtolea maneno machafu mkuu
huyo wa wilaya baada ya kumtaka aachie ngazi ya uongozi baada ya kuhukumiwa
kifungo cha nje kwa mwaka mmoja na mahakama.
TAZAMA VEDEO MKUU WA WILAYA AKATATIWA KUFANYA KAZI NA CHADEMA.................
Post a Comment
Post a Comment