KAMATI ya bunge ya Madawa ya Kulevya na Ukimwi imetoa agizo kwa vituo vya huduma endelevu kwa waviu Mkoa wa Njombe kutoa huduma bora kwa wateja wao ili kupunguza watu wanaotoroka kuchukua dawa kutokana na kauli mbovu za wahudumu.
Kamati hiyo ikiwa mkoani Njombe katika ziara yake ya siku moja inapita katika vituo viwili vya kutolewa huduma wa Waviu na kuzungumza na watu hao ambao wanalalamikia watoa huduma kuto kuwa na Lugha nzuri kwa wateja hao na kutoa maagizo sita kwa serikali ili kuhakikisha huduma zinaboreshwa.
Mwenyekiti wa muda wa kamati hiyo Dr. Haji Mponda anatoa maagizo sita baada ya kutembelea vituo na kukutana na waviu mkoani Njombe ikiwemo serikali kuwa na ushirikiano na vituo binafsi vinavyotoa huduma kwa jamii, kuhakikisha dawa, vitendanishi na Kondomu zinasambazo katika vituo binafsi.
Wajumbe wa kamati hiyo wanakuwa na maswali kwa serikali mkoani Njombe kuhusu utoaji wa huduma kwa vijana na ushwawishi wa upimaji wakiwa katika kituo cha kutolewa huduma cha binafsi cha mjini Makambako.
Awali wakisoma taarifa wakuu wa vituo wanasema kuna changamoto mbalimbali katika kutoa huduma kwa waviu.
Serikali na watumishi wa idara za afya wanatoa ufafanuzi kwa yale waliyoyatoa wabunge wajumbe wa kamati.
Kutokana na changamoto hizo pamoja na kuwasikiliza waviu ambao nao waliyonayao moyoni huku wakilalamikia kuwa na vikundi visivyo saidiwa kupata fedha serikalini kwaajili ya kuendeleza shughuli za kuwaongezea kipato ndicho kilicho isukuma kamati hiyo kutoa maagizo.
TAZAMA KAMATI YA BUNGE ILICHO AGIZA IKIWA NJOMBE.........................
Post a Comment
Post a Comment