MKUU wa mkoa wa Njombe amemwagiza mfanyabiashara anayefanya ujenzi katika eneo la Airport halmashauri ya Mji wa Njombe ambaye anaendelea na ujenzi wa Ghorofa karibu na uwanja huo mpaka wataalamu wa anga kutoa maelezo.
Anatoa kauli hiyo akiwa katika eneo hilo baada ya kutembelea ambapo mfanyabiashara huyo aliuliza kwa watu wanaofanya tathimini kwa watu wanao takiwa kulipwa fidia karibu na maeneo hayo ambapo inadaiwa kuwa aliambiawa eneo lake halina madhara kwa uwanja wa ndege.
Uwanja huo wa ndege unatarajiwa kufanyiwa upanuzi kwa kuwaondoa wakazi walio mbele na nyuma ya uwanja huo ili kuto ingilia shughuli za utuaji na upaaji wa ndege kiwanjani hapo.
Mfanyabiashara huyo ambaye anakutana na mkuu wa mkoa anaweka bayana kuhusu ujenzi wake na kuwa anavibali kutoka mamlaka zinazohusika na ujenzi.
Mkuu wa mkoa anatoa agizo la kusimama kwa ujenzi huo ili kusuburi tathimini za wataalam juu ya madhara yatakayo tokea kutokana na kuwapo kwa jengo refu katika eneo hilo.
Meneja wa viwanja vya ndege mikoa ya Njombe na Iringa, Hana Kibopile anasema kuwa kiwanja hicho kipo katika mpango wa kukarabatiwa.
TAZAMA KILICHO SEMWA NA MKUU WA MKOA HAPA CHINI........................
Post a Comment
Post a Comment