const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); TZ TOWN MKUU WA WILAYA AMUWEKA NDANI MASAA 48 MWENYEKITI WA MTAA - HABARI MPYA

..

TZ TOWN MKUU WA WILAYA AMUWEKA NDANI MASAA 48 MWENYEKITI WA MTAA

Post a Comment
MKUU wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amemuweka ndani masaa 48 Aliye kuwa mwenyekiti wa mtaa wa Buguruni kata ya Njombe Mjini halmashauri ya Mji wa Njombe Emmanuel Ngelime baada ya kutakiwa kuachia madaraka kutokana na kile kinachodaiwa kuwa amehukumiwa kifungo cha nje kwa miezi 12 na kutoa maneno machafu kwa mkuu huyo wa wilaya.

Mkuu wa wilaya anasema kuwa sheria inasema kiongozi yeyote akihukumiwa miezi zaidi ya sita anakuwa hana nafasi ya kuwa katika ofisi ya umma lakini kiongozi huyo alihukumiwa kifungo cha nje kwa miezi 12 tangu mwaka jana lakini inadaiwa kuwa bado yupo ofisini.
Akizungunza na Startv mkoani Njombe Msafiri anasema kuwa alifika katika eneo la mtaa huo kwajili ya kumtaka mwenyekiti huyo Emmanuel Ngelime kuachia ngazi hiyo lakini alikutana na kauli mbovu na kuagiza askali kumuweka ndani.

Anasema kuwa kiongozi yeyote akihukumiwa kifungo cha miezi zaidi ya sita kile uongozi wake unakomea palepale.
Amesema kuwa baada ya masaa hayo 48 kama atakili kosa anamwacha na kama hatakili basi kuna hatua zitachukuliwa baada ya kushauriana na kamati ya ulinzi na usalama.
TAZAMA VIDEO MKUU WA WILAYA AMUWEKA NDANI ALIYE KUWA MWENYEKITI WA MTAA................

Related Posts

Post a Comment