const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); TzTown Tv: TAZAMA VIDEO WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO WANAWEZA KUPONA KWA MAZOEZI - HABARI MPYA

..

TzTown Tv: TAZAMA VIDEO WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO WANAWEZA KUPONA KWA MAZOEZI

Post a Comment
WATOTO wenye Utindio wa Ubongo wakipatiwa mazoezi wanaweza kuimarika katika afya zao za akili na kuwa na utendaji kama mtu mwingine yeyote huku wazazi hapa nchini wakitakiwa kuwatambua mapema watoto wao wenye matatizo.
Pamoja na kudaiwa kuwa wanaweza kupona inaelezwa kuwa kila pahara hapa ulimwenguni kuna watu wenye utindio wa Ubongo mkurugenzi wa Special Olympic Tanzania, Charles Dennis anasema kuwa kila watu 10 watu watatu wana utindio wa ubongo.
Anatoa kauli hiyo wakati akitoa mafunzo kwa wazazi wa watoto wenye utindio wa Ubongo Mkoani Njombe ambapo anasema kuwa mazoezi kwa watoto hao ni dawa ya kuwaweka sawa na kupona kabisa.
Anasema kuwa ulimenguni kote watoto walio gundulika mapema wamefanyiwa mazoezi na kuwa sawa na kufanya kazi kama watu wengine ambao hawana utindio wa ubongo.
“Kuna muhudumu wetu ambaye alikuwa na utindio wa Ubongo baada ya mazoezi ya kutosha sasa yupo zizuri na anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni,” alisema Dennis.
Aliongeza kuwa kuna kijana pia ambaye alipelewa kushindana na uongozi wa Special Olymipic; “Kijana huyo amefanikiwa kwenda Marekani kwenda na kurudi bila kupotea lakini kuna watu huwa wanapotea wakati hawana utindio wa Ubongo.” 
Mwenyekiti wa Bodi ya Special Olympic Mwanandi Mwankemwa anasema kuwa watoto wenye utindia wa Ubongo akipatiwa mazoezi ya kutosha ataweza kupona.
Alisema kuwa watoto wenye utindio wa Ubongo haupaswi kufichwa kwa kuwa watoto hao wanapo fichwa wananyimwa haki zao.
Wazazi nao wanakili kuwapo kwa mabadiliko baada ya watoto wao kupatiwa mazoezi na wemeanza kuonyesha ushirikiano tofauti na awali walivyo kuwa kabla ya kupatiwa mazoezi.
Licha ya kuwapo kwa faraja kubwa wanayo ipata baada ya kupatiwa elimu ya kutoa mazoezi kwa watoto lakini kuna wanajamii ambao wanawanyanyapa kutokana na kuwa na watoto wa aina hiyo.
Ferista Magumbuli ni mzazi anaomba serikali kuboresha mazingira ambayo watoto hawa wanaenda kusoma ili kuto pata shida wakiwa shuleni kwa kuwa mazingira ya shule hayapo rafiki na watoto hao hasa vyooni.
Inadaiwa kuwa utindio wa ubongo unatokana na matatizo mbalimbali wakati wa kuzaliwa na wakiwa na umri mdogo wazazi wanatakiwa kuwatambua watoto wao wakiwa wadogo na kutibu maradhi ya kifafa kwa watoto ili kuto endelea kuwaathili akili zao.

TAZAMA VIDEO WATOTO WENYE UTINDIO WA UBONGO WANAWEZA KUPONA KWA MAZOEZI..............

Related Posts

Post a Comment