MWENYEKITI wa kitogozi cha Ifuna kijiji Cha Utalingolo halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe Kastor Ngauliwa ameuwawa mita chache kutoka nyumbani kwake na watu wanaosadikika kuwa ni ndugu baada ya kuhisi kuwa ni mchawi.
Wananchi na viongozi wa kijiji hicho wanasema tukio hilo limewakumba watu wawili huku mmoja akijeruhiwa wakati akimsaidia marehemu kabla ya kuuwawa.
Ni kilio na majonzi katika kijiji Cha Utalingolo ambako mwenyekiti wa kitongoji ameuwawa wa tuhuma za ushirikina.
Diwani wa kata ya Utalingolo Filbert Njawike na baadhi ya viongozi wa kiserikali wanasema kuwa aliye kuwa akimsaidia marehemu Ado Njawike alifanikiwa kuwatoroka wauaji.
Taarifa za kifo cha Mwenyekiti huyu na kujeruhiwa kwa mtu aliye kuwa akimsaidia zinathibitishwa kwa njia ya simu na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Prudensiana Protas.
Tazama Video Hapa....................
Post a Comment
Post a Comment