HALMASHAURI ya mji wa Njombe imesema kuwa itasaidia wananchi ambao watakuwa tayari kujisaidia katika kuvumbua miradi na halmashauri itatia mkoni wake kusaidia wananchi hao.
Kauli hiyo inatolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Njombe wakati akizidua Zahanati ya kijiji cha Iduchu ambayo ilianzwa kujengwa na wananchi wa kijiji hicho kwa zaidi ya miaka mitano iliyo pita.
mkurugenzi anasema kuwa serikali itachangia haraka na kuwataka wananchi hao kuanza ujenzi wa nyumba ya Mganga mkuu wa Zahanati yao.
Diwani na mwenyekiti wa kijiji wanasema kuwa ujio wa Zahanati hiyo ni kama baraka kwao.
Wananchi wanasema kuwa wamekuwa wakitibiwa mbali na makazi yao na kuwa baada ya kuzinduliwa kwa zahanati hiyo watatibiwa jirani.
Katika zahanati hiyo kumepekekwa dawa kwaajili ya kuanza matibabu, kitanda mzani na vifaa vingine muhumu vya kutolea huduma za afya.
Tazama video hapo chini
Post a Comment
Post a Comment