IMEDAIWA kuwa watanzania asilimia kubwa bado hawana elimu juu ya faida za kununua hisa na kusababisha watu wachache wanao nunua hisa na wengine kubaki bila kuwekeza wakati Makampuni yanauza hisa.
Hata hivyo Madalali wa uuzaji na ununuzi wa hisa wakiombwa kufungua ofisi zao katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuwafikia hata wananchi walioko maeneo ya vijijini na kuwekeza katika Fulsa za uwekezaji katika kumiliki kampuni zinazo uza hisa zinazoingia na zilipopo katika soko hilo ndani na nje ya nchi.
Hayo yanabainika katika mkutano wa pamoja kati ya wamiliki na wafanyakazi wao wa Banki ya CRDB mkoani Njombe ambapo madalali wa Hisa hapa nchini wametakiwa kusambaa nchi nzima ili watanzania kuwekeza katika Kampuni mbalimbali kwa kununua hisa.
Je nini Mununuzi wa hisa anatakiwa kuangalia kabla ya kuwekeza kwa ununuzi wa hisa? Emmanuel Hauli ni mkufunzi anatoa ufafanuzi.
Wanahisa atafata faida kulingana na kampuni aliyo wekeza inavyopata faida na kuwa kampuni inapandisha thamani ya hisa kutokana na faida ya kampuni kwa mwaka inavyo panda.
Hapa nchini kuna soko moja la hisa la Dar es salaam ambalo linamamlaka ya kuziingiza kampuni kuuza hisa hapo ambapo mnunuzi atanunua hisa huko kupitia madalali mbalimbali ambao wanauza hisa kwa bei iliyopo sokoni kulingana na kampuni husika, na sasa kampuni za simu zimetakiwa kuuza hisa zao ili nao watanzania kuwa na umiliki katika kampuni hizo.
WANAHISA WAPATA ELIMU...................
Post a Comment
Post a Comment