WAKAZI wa mtaa wa Ramadhani Mjini Njombe baada ya kuona watoto wao wanatumia vyoo vilivyo hatari kwa afya zao wameamua kujenga vyoo vya kisasa vilivyo garimu zaidi ya shilingi milioni 22 kutoka mifukoni mwao katika shule ya msingi Ramadhani Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo.
Vyoo hivyo baada ya kukamilika wameamua kuikabidhi kamati ya shule hiyo ili kuanza kutumika na watoto wao na kuachana na vile vyoo vya zamani vya shimo ambavyo walikuw awakitumia hapo awali.
Ni katika mkutano wa hadhara wa mapato na matumizi inaelezwa kuwa zaidi ya milioni 22 zimetumika katika ujenzi wa vyoo kwaajili ya watoto wanao soma katika shule ya msingi Ramadhani ikiwa ni micnango ya wananchi kwa asilimia 100.
Wazazi na viongozi wa mtaa huo wanasema kuwa walikuwa watoto wao walikuwa hatarini kupatwa na magonywa ya mripuko kutokana na kutumia vyoo visivyo salama.
Naye mkuu wa shule hiyo anasema kuwa baada ya kukabidhiwa vyoo hivyo sasa wanafunzi wataepuka magonjwa yatokanayo vyoo visivyo bora pamoja kuwapo kwa uhaba wa matundu kulindana na idadi ya wanafunzi.
Vyoo walivyo kuwa wakitumia wanafunzi wa shule hii ni vya shimo lakini harufu inayo toka humo ni kali pamoja na kuwapo kwa hajandogo pembeni ya mwashimo ya vyoo huku uchafu ukijazana pembeni ya matundu.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI VYOO VILIVYO KABIDHIWA NA LINGANISHA VYA ZAMANI NA VIPYA...................
Post a Comment
Post a Comment