BAADHI ya wakazi mjini
Njombe wasmekosoa mfumo wa utoaji wa mikopo kwa vikunndi vya wakina mama na
Vijana kutokakatika mapato ya halmashauri yaliyo kusanywa kwa muda wa robo ya
kila mwaka wa fedha ikiwa ni asilimia kumi ya makusanyo.
Wanasema kuwa utoaji
wa mikopo hiyo kwa vikundi umejaa Usiri pamoja na kudaiwa kuwa elimu kwa
vigundi na vijana haijatolewa ili kuvijua vigezo vya kupata mikopo hiyo.
Wakizungumzia utoaji
wa mikopo hiyo Mbele ya Kamera Tz Town Tv kwa vijana na wakina mama baadhi ya wakazi wa mji huu wanasema
kuwa wanahitaji mikopo hiyo lakini jinsi ya kupata ni kiza.
Licha ya kudaiwa kuto
kuwapo kwa elimu kwa wanufaika wa mikopo na kuto jua jinsi ya kuipata
halmashauri ya mji wa Njombe imetoa Mkopo kwa vikundi 51 wenye thamani ya milioni
106 ikiwa ni asilimia kumi tu ya mapato yake kwa robo hii.
Wananchi wanahimizwa
kulipa kodi ili asilimia hizo kupatikana wito ambao unatolewa na mwenye
halmashauri hiyo ambapo anakabidhi hundi hiyo ya zaidi ya milioni 100.
Wanaochukua mkopo huu kupitia Saccos za za
maeneo yao wanasema Mbele ya kamera ya TzTown Tv hapo chini
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI VIJANA WAPOKEA MAMILIONI..............
Post a Comment
Post a Comment