WAKULIMA wa zao la viazi Mviringo, Mkoani Njombe wameendelea kupatiwa elimu ya kilimo bora cha viazi mviringo kwa kutumia zana bora na za kisasa za kupanda,kuweka mbolea kuweka matuta na kuvunia.
Teknolojia hiyo ambayo itawawezesha wazalishe kwa tija tofauti na kilimo cha jembe la mkono walicho kuwa wakikifanya hapo awali.
Elimu hiyo ya kilimo bora imeanza kutolewa na mpango wa uendelezaji wa kilimo nyanda za juu kusini SAGCOT kwa kushirikiana na serikali mkoani Njombe,na sekta binafsi ambapo kwa kuanza wakulima wa kata ya Mtwango wamepatiwa elimu hiyo kwa vitendo katika shamba la Matanana farm lenye ukubwa wa hekta kumi liloandaliwa na wakulima wenyewe wa kata ya Mtwango walioko katika vikundi takribani 13 vyenye jumla ya wanachama 250.
Viongozi wa serikali nao wanaimani na hatua hiyo ya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Zana bora na za kisasa kuwa kama ikifuatwa itawakwamua wakulima kwa kuongeza kipato kama anavyoeleza
Kwa upande wao wakulima wa zao la viazi Mviringo wanasema kuwa tangu mradi huo uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita mavuno yao yameongezeka na matumizi ya zana bora na za kisasa yatawafanya kuwa na uwezo wa kumiliki mashamba makubwa pamoja na kutoa ajira kwa wengine.
Mradi huu wa Uzalishaji na Usambazaji wa Mbegu bora ya Viazi mviringo, unatekelezwa mkoani njombe katika halmashauri tatu za Wanging’ombe,Njombe mji,na Halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa Ufadhili wa serikali ya watu wa Marekani USAID, kupitia shirika la Kimataifa la Mapinduzi ya Kijani, AGRA
Tazama Video hapa Chini...............
Post a Comment
Post a Comment