KIWANDA kinacho tengeneza mafuta ya kukinga mionzi ya Jua kwa watu wenye Ualbino cha Mjini Moshi kinakabiliwa na changamoto ya kupata marighafi kwaajili ya utengenezwaji wa Mafuta hayo ambayo yanagawanywa bure kwa watu wenye Ualbino.
Kwa mujibu wa Peter Kundi, Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya Ngozi Hospitali ya KCMC Moshi anasema kuwa marighafi ni adimu kwa kiwanda cha kutengeneza mafuta hayo ambayo yakitengenezwa hutolewa bure kwa madhumuni ya kujikinga na mionzi ya juu inayo wasababishi kansa.
Serikali nayo inampango wa kuhakikisha kuwa mafuta hayo yanapatikana katika Hospitali zote mpaka Zahanati Nchi Nzima ili watu hawa wasipate shida ya kuyapata.
Kauli hiyo imetolewa na waziri huyo hivi karibuni wakati wa Maadhimishi wa Kimataifa ya siku ya Albino Duniani ambayo kitaifa yamefanyika Mjini Dodoma na kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini na Ulimwenguni.
TAZAMA OMBI LA KIWANDA CHA MAFUTA YA KUZUIA MIONZI KWA SERIKA,LI HAPA CHINI.....................................
Post a Comment
Post a Comment