KATIKA kuhakikisha kuwa kila halmashauri inakuwa na kitega
uchumi Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe inatarajia kuaza
ujenzi wa soko la kubwa kwaajili ya biashara ya Nyanya na kuwasaidia wakulima
kupata mahara pa kuuzia nyanya.
Halmashauri hiyo imebaini kuwa kuna wakulima wao wengi
wanalipa ushuru katika halmashauri Nyingine wakati wao wanauwezo wa kuwa na
soko la nyanya na wakapata maendeleo kutokana na pesa zao za Ushuru wa Mazao.
Mradi huo umebuniwa na halmashauri ya wilaya hiyo katika
vikao vyake vya halmashauri lakini kinacho wakwamisha mi mtaji wa ujenzi wake
Mwenyekiti wa halmashauri Hiyo anasema ujenzi unategemea mapato ya Ndani.
Hata hivyo diwani wa eneo linapotakiwa kujenga soko hilo
anakili kuwapo kwa bajeti ndogo ya mapatio ya ndani ya halamashauri kwajili ya
ujenzi wa soko hilo.
Kutokana na bajeti Ndogo nini inatarajia kufanya halmashauri
kama mpango wa awali kuanzisha soko hilo
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa mkoani Njombe hivi karibuni anazitaka halmashauri
kujitafutia vyanzo vya mapato ili kujiinulia kupato na kutoa huduma bora kwa
jamii
Post a Comment
Post a Comment