const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); IDARA YA UHAMIAJI YAELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA MAKWAO BAADHI YA RAIA WA KIGENI - HABARI MPYA

..

IDARA YA UHAMIAJI YAELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA MAKWAO BAADHI YA RAIA WA KIGENI

Idara ya uhamiaji nchini imeagiza kurudishwa makwao, zaidi ya wahamiaji haramu 100 waliokuwa wakiishi nchini tangu mwaka 1972 pasipokuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Kilimanjaro, imeeleza kuwa wahamiaji 94 kati ya hao, wanaweza kurudi kuendelea kuishi nchini pale tu watakapofuata taratibu za kisheria ili kupata vibali.


Kati ya wahamiaji hao, 71 ni raia wa Kenya, 7 wa Rwanda, 7 ni wa Congo, 5 wa Ethiopia, 1 wa Somalia na mwingine mmoja ni raia wa Nigeria.

“Tumegundua kwamba baadhi ya wahamiaji hawa, waliingia nchini mwaka 1972 na wamekuwa wakiishi hapa pasipokuwa na kibali. Tumewarudisha makwao, na kama wanataka kurejea kuishi hapa nchini, basi wafuate utaratibu,” alisema Albert Rwelamira, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro.

Aliongeza kuwa wengi wao walikuwa wana ndoa na watanzania pamoja na familia. Wahamiaji 23 kati ya waliorudishwa wamenyimwa vibali vya kurudi kuishi hapa nchini.

Related Posts

Post a Comment