Watu 12 wameshtakiwa nchini Sierra Leone kwa tuhuma za kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa la Novemba 2023.
Washtakiwa hao wanajumuisha polisi wa zamani na maafisa wa kurekebisha tabia na pia mlinzi wa zamani wa Rais wa zamani Ernest Bai Koroma. Koroma amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu alipohojiwa na polisi mwezi uliopita.
''Washukiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na uhaini, kuficha uhaini na kumhifadhi, kumsaidia na kumfadhili adui," Waziri wa Habari Chernor Bah amesema katika taarifa yake.
Washukiwa wengine "wanatarajiwa kushtakiwa katika siku zijazo," aliongeza.
Tarehe 26 Novemba, watu wenye silaha walivamia ghala la kijeshi na magereza kadhaa katika mji mkuu wa Freetown, na kuwaachilia huru karibu wafungwa 2,000.
Takribani watu 19 wakiwemo wanajeshi 13 walifariki katika ghasia hizo, ambazo zilitajwa kuwa ni jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililoshindwa.
Mwezi Disemba, serikali ilitangaza inawashikilia washukiwa 80 wa jaribio hilo la mapinduzi, wakiwemo raia na maafisa wa polisi na wanajeshi wa zamani.
Binti wa Koroma, Dankay Koroma, pia alitajwa miongoni mwa washukiwa wengine 54.
Post a Comment
Post a Comment