const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); TAPSEA watoa misaada kwa waathiriwa wa Maafa Hanang' - HABARI MPYA

..

TAPSEA watoa misaada kwa waathiriwa wa Maafa Hanang'


Na John Walter-Manyara

Umoja wa Makatibu Muhtasi (TAPSEA) mkoa wa Dodoma, wametoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi Milioni tano kwa ajili ya waathiriwa wa maporomoko ya tope mawe na Magogo.

Mwakilishi wa Makatibu Muhtasi kutoka Dodoma Conjeta Chambila amesema kwenye zawadi walizotoa wamegusa watoto wa shule na wanawake  ambapo wamepeleka Vitambaa majora matano kwa ajili ya kushona sare za shule, madaftari, kalamu, penseli, na nguo mchanganyiko.

Katibu tawala wilaya ya Hanang' Athuman Likeyekeye akipokea misaada hiyo amesema itawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa huku akiwapongeza Makatibu hao kwa moyo wa upendo waliounyesha kwa waathirika wa maafa hayo yaliyoacha majonzi.

Katibu Muhtasi ofisi ya katibu mkuu wizara ya jenzi Devotha Mbuya na Habiba Mhina kutoka TAPSEA mkoa wa Dodoma, wamesema waliamua kujichanga kwa pamoja walichonacho ili kutoa pole kwa wote waliokumbwa na janga hilo pamoja na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa wa kwanza kuonesha kujali Wananchi wake kwa kuelekeza serikali ihamishie nguvu Hanang kuwasaidia waathiriwa.

Aidha makatibu hao wamemshukuru na kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour kwa kuwapatia usafiri uliowawezesha kufika wilayani Hanang' na kutembelea maeno yote yaliyoathiriwa na maafa hayo yaliyotokea Desemba 3, 2023 na kusababisha vifo vya watu 89 na majeruhi 139.

Related Posts

Post a Comment