SERIKALI imeipongeza Kampuni ya Bima ya First United Takaful kwa kuanzisha huduma za kibima zitakazoweza kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwa ujumla pamoja na sekta ya fedha ya mwaka 2020 mpaka 2030 inayotoa dira kwa sekta ndogo ya bima sambamba na maelekezo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar.
Pongezi hizo zilitolewa na jana Januri 30,2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Uchumi wa Zanzibar, Dk. Saada Mkuya wakati akizindua kampuni hiyo pamoja na huduma ya bima ya Takaful inayofuata misingi ya dini ya kiislamu jijini Dar es Salaam jana akisema uzinduzi huo unaunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta ya bima.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE
Post a Comment
Post a Comment