Na Bilgither Nyoni
Wazazi na walezi wa halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wametakiwa kuwaandikisha watoto wenye umri wa miaka mitano kwa ajili ya kuanza darasa la awali kwa mwaka wa masomo 2024.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa elimu msingi halmashauri ya mji wa makambako Mwalimu Yusto Nyamle,wakati akizungumza na Ice fm juu ofisini kwake juu ya umuhimu wa elimu ya awali ambapo amesema Uandikishwaji wa watoto wa awali ni wa kusua sua hivyo amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wote wenye umri wa kuanza shule hasa darasa la awali na darasa la kwanza kwakuwa Serikali imeweka miundombinu rafiki kwa ajili ya watoto kupata elimu.
“Kwa wazazi wote ambao Bado hawajawaandikisha watoto wao ambao wamefikia umri wa kuanza shule basi wafike katika shule iliyopo jirani na yeye ili kumuandikisha mtoto wake ambapo kwa darasa la awali umri ni miaka 5 hadi 6 na kwa darasa la kwanza umri ni miaka 7 hivyo natoa rai kwa wazazi na walezi wote muda kwa muda huu uliosalia kuandikisha watoto ili waanzekupata elimu”
Aidha mwalimu Myambe amesema, matarajio ya Halmashauri ni kusajili watoto 4114 kwa darasa la awali, na mpaka sasa wamesajili watoto 2217 sawa na asilimia 54.
Geofrey Lungwega Ni mdau wa elimu katika halmashauri ya mji wa makambako amesema kusua sua kwa undikishaji wa watoto ambao wanatakiwa kujiunga na elimu ya awali ni kutokana uelewa mdogo wa wazazi juu ya umuhimu wa awali.
Nao baadhi ya wakazi wa mji wa makambako wamesema kuwa kusua sua kwa baadhi ya wazazi kuwaandikisha watoto darasa la awali ni uelewa mdogo juu ya umuhimu wa elimu hiyo
Kufuatia mkakati wa uboreshaji wa Elimu wa mwaka 2022 uliazimia watoto wa awali na darasa la kwanza waandikishwe kuanzia tarehe 1 Octoba hadi tarehe 31 Disemba na utekelezaji wake umeanza rasmi mwaka huu wa 2023 ili ifikapo januari 2024 watoto waanze masomo kwa kuingia darasani.
Post a Comment
Post a Comment