const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT aongoza zoezi la upandaji miti Makao Makuu JKT Dodoma - HABARI MPYA

..

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT aongoza zoezi la upandaji miti Makao Makuu JKT Dodoma


 Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa JKT Dkt. Stergomena Tax amewaongoza JKT katika zoezi upandaji miti Makao Makuu ya JKT Wilaya ya Chamwino Dodoma huku akisisitiza usimamizi wa miti ianayoendelea kupandwa kupitia kampeni mbalimbali nchini.

Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo Waziri Dkt Stergomena Tax amesema kuna miti mingi inapandwa kupitia kampeni mbalimbali lakini matokeo hayalingani na zoezi linalofanyika.

“Sehemu nyingi miti inapandwa lakini inatelekezwa na inakauka na tunatumia lasilimali nyingi na inapotea ni vyema uwekwe utaratibu wa usimamizi wa miti inayopandwa ili matokeo yaweze kuonekana”

Tunapoanza kampeni mpya ya kupanda miti katika msimu mpya ni vyema tukatathmini miti iliyopandwa msimu iliopita ili kujua udhaifu kupitia kampeni iliyopita ili kurekebisha kupitia kampeni mpya” amesema


Katika hatua nyingine amepongeza zoezi hilo na kusema Jeshi litakuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutoa rai kuhakikisha jamii inaona umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti onyo na kupanda miti.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa JKT ambaye pia ni Mkuu wa tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema JKT itaendelea kushiriki kwa vitendo zoezi la kupanda miti katika makambi yote ya JKT ili kulinda mazingira.

“Zoezi hili linaloendelea hapa linafanyika katika vikosi vyote vya JKT na zoezi hili tunalichukulia kwa uzito lengo ni kuhakikisha tunapanda miti ya kutosha ili kulinda mazingira yetu na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi” amesema.

Amesema kwa mwaka 2023 JKT ilipanda miti zaidi ya elfu 75800 imepandwa katika maeneo mbalimbali na kwa mwaka huu tumepanga kupanda miti zaidi ya 100000 katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pia amebainisha kuwa JKT imeanza kutii agizo la Serikali la taasisi zenye watu zaidi ya laki moja kuacha kutumia nishati ya kuni na mkaa kwa kuanza kutumia nishati mbadala kwa kuacha kutumia kuni lengo likiwa ni kutunza mazingira huku wakiendelea kupanda miti.

Akishiriki zoezi hilo Naibu Waziri wan chi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira mhe. Khamis Hamza Khamis ameipongeza JKT kwa kuona umuhimu wa kupanda miti ili kulinda mazingira na kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Related Posts

Post a Comment