News
Njombe
Serikali kupitia wakala wa mbegu za kilimo ASA imekabidhi bure tani elfu moja za mbegu ya Ngano yenye thamani ya Bilioni nne kwa ajili ya msimu wa kilimo kwa wananchi wa mkoa wa Njombe kwa kuanza na wilaya ya Makete kwa lengo la kuongeza tija na kukuza uzalishaji wa zao hilo nchini ambapo wilaya ya Makete inatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa ngano kutokana na ardhi ya wilaya hiyo kukubali kwa kiasi kikubwa zao la Ngano ambapo pia ni utekelezaji wa awamu ya pili wa mkakati kabambe kwenye uwekezaji wa zao la Ngano wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka mara baada ya kupokea mbegu hizo zilizofikishwa wilayani humo na Jeshi la wananchi amebainisha kuwa serikali ya mkoa huo itahakikisha usimamizi mzuri kwenye zao hilo ili kutimiza adhma ya serikali ya kupunguza uagizaji wa Ngano kutoka nje ya nchi huku akitoa wito kwa wananchi hususani wa wilaya ya Makete kuchangamkia fursa ya kilimo hicho.
"Kilo moja ya mbegu ya Ngano ni shilingi elfu nne na tumepewa tani elfu moja ambazo ni sawa na kilo elfu kumi ukizidisha mara nne ni sawa na Bilioni nne na hii ngano imetolewa bure ili watu wa Makete walime lakini ASA watakuwa tayari kununua kwa wananchi watakaopanda kwa ajili ya mbegu lakini watu wengine watanunua kwa wale wananchi ambao wamelima ngano kwa ajili ya chakula"amesema Mtaka
Meneja wa shamba la ASA Dabaga mkoa wa Iringa Nicholaus Msangi kwa niaba ya mtendaji mkuu wa ASA Dkt,Sophia Kashenge amesema mbegu waliyokabidhi ina sifa zote ikiwemo kuwahi kukomaa na yenye mazao bora hivyo ametoa wito kwa wakulima kukimbizana na msimu wa kilimo na kupata elimu ya kutosha ili kupata mavuno bora.
"Sisi tunaishukuru sana serikali kwa kusaidia kupatikana tani hii elfu moja na ni bure kabisa,sisi tumeleta ngano na wakulima kazi yenu ni kulima na kuvuna ila tunawashauri wakulima tuangalie muda kwa kuwa tunapaswa kulima miezi ya mitatu ya mwisho ya mvua tutapatab ngano bora bila kulalamika"amesema Msangi
Josaya Luoga ni Mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe kwa niaba ya chama hicho ameipongeza serikali kuona umuhimu na jitihada za kuzalisha ngano kwenye wilaya hiyo kwa kuwa ina hali ya hewa inayokubali mazao mengi ambapo pia eneo hilo linaouwezo wa mkubwa wa kuzalisha nusu ya mahitaji ya Ngano nchini.
Post a Comment
Post a Comment