Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi kimesema kimewalipa wakulima wa korosho waliouza kupitia minada nane kati ya tisa iliyofanyika katika nsimu wa 2023/2024.
Hayo yalielezwa jana na kaimu wa kaimu meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Emmanuel Wilbard alipozungumza na Muungwana katika ofisi kuu ya chama hicho iliyopo mjini Nachingwea.
Emmanuel ambaye ni meneja masoko wa chama hicho alisema katika msimu wa 2023/2024 chama hicho ilifanyika minada tisa ya korosho ghafi. Ambapo malipo ya wakulima waliouza korosho kupitia minada nane wamefanyika.
Alisema wakulima ambao hawajalipwa watakuwa ni waliouza korosho zao katika mnada wa tisa ambao ulifanyika mwezi Disemba 2023.
Alitaja sababu ya wakulima waliouza korosho katika mnada wa tisa kutolipwa kuwa ni baadhi ya korosho kukosa wanunuzi. Kwani hadi sasa zimebaki. Nakwamba sehemu ya korosho zilizo nunuliwa katika mnada huo fedha zake wamelipwa baadhi ya wakulima ambao waliuza katika mnada huo.
Alibainisha kwamba kama kuna wakulima ambao hawajalipwa baada ya kuuza katika minada mingine mbali ya mnada wa mwezi Disemba 2023 basi changamoto hiyo haijasababishwa na RUNALI. Bali vyama vyao vya msingi vya ushirika(AMCOS) havijapeleka taarifa za wakulima hao kwa chama kikuu au wamesababisha wakulima wenyewe.
" Wakulima wamelipwa minada yote nane. Hata mnada wa tisa baadhi wamelipwa. Bali mnada wa tisa baadhi ya korosho hazijauzwa. Lakini minada mingine yote wakulima wamelipwa. Au uhenda kunarijeksheni," alisisitiza Emmanuel.
Ofisa huyo wa RUNALI alitoa wito kwa wakulima ambao hawajalipwa hadi sasa wahakiki akaunti zao kama taarifa zao zipo sawa sawa na hazijalala. Lakini pia wawasiliane na viongozi na watendaji wa AMCOS zao ili wahakiki kama taarifa zao zilitumwa katika chama kikuu hicho.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wakulima wa korosho kwamba hawajalipwa fedha zao. Ingawa waliuza korosho zao miezi ya Oktoba na Novemba 2023.
Malalamiko ya wakulima ndio yaliyosababisha Muungwana Blog kwenda katika ofisi za RUNALI ili kujua ukweli wa malalamiko na madai hayo ya wakulima.
Post a Comment
Post a Comment