Na TImothy Itembe Mara.
Kaimu Meneja Ruwasa wilaya Tarime,Mohamed Mtopa alisema juzi kwenye kikao Cha tadhimini Cha wadau wa maji kuwa RUWASA Tarime wametekeleza miradi 19 Kwa mwaka 2023 inayotoa maji Kwa vijiji vyote wilayani humo.
Mtopa aliongeza kuwa mwaka huu wa fedha tuna miradi 4 ambayo tumepanga kuitekeleza Kwa vijiji vyote ambapo Kwa sasa tuna wastani wa uzalishaji wa maji asilimia 73.3 Kwa miradi iliyokamilika.
Pia tuna miradi sita ambayo ikikamilika tutakuwa na wastani na uzalishaji asilimia 76 hivyo basi tunalengp kuwa kufikia mwaka 2025 kufikia asilimia 85 kama lengo la Serikali inavyosema.
"Katika kuondoa changamoto inayolalamikiwa wateja kubambikiwa bili ya maji na ujanja ujanja kwenye mita na upotevu wa maji timepata kampuni ya wazawa WAZO Pick Kwa lengo la kutuuzia mita Bora na za kisasa ambazo zitakuwa suluhisho na tunaendelea na mazungzo"alisema Afisa huyo.
Kwa upande wake mgeni rasimi wa kikao hicho,katibu Tawala wilaya Tarime,mwalimu Saul Mwaisenye alisema Kwa niaba ya mkuu wa wilaya Michael Myenjele ambaye alikuwa amealikwa kuwa viongozi na wadau wa maji wanatakiwa kilinda na kutunza miradi inayotekelezwa ikiwemo kutunza na kilinda mazingira ili kudumu Kwa mahitaji ya vizazi vyoye vilivyopo na vijavyo.
Mwaisenye alitumia nafasi hiyo kuzitaka mamlaka zinazo husika kuacha Tabia ya kuwabambikia wateja wao bili ya maji kwasababu haiwezekani mtu kudaiwa kulipa bili ya maji ambayo hajatumia.
Mkurugenzi wa kampuni ya Wazawa,WAZO pick,Peter Masubo Mwita alisemawamekuja na mita za maji ambazo zitakuwa suluhisho kwa watumiaji na mamlaka kwani mita hizo Zina sifa nyingi ikiwemo kuratibu mfumo wa maji uliotimia unanunua tokeni mfano kama watumiaji wa umeme na hakuna ujanja wa wizi katika mita hiyo.
Naye Afisa ufuatiliaji na tadhimini na mafunzo kutoka shirika la WWF,Enock Edward alisema wanatoa elimu katika utunzaji na kilinda vyanzo vya maji jamii inatakiwa kufuga nyuki kwenye miti iliyopo kwenye vyanzo hivyo badala ya kukata miti na elimu HII imesaidia kilinda na kutunza vyanzo vya maji.
Post a Comment
Post a Comment