Wahitimu wa mafunzo katika ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wamehimizwa kuishi kwa nidhamu na kutambua thamani zao kwani Serikali inawajali katika kuboresha hali zao za kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo Desemba 8,2023Jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akifunga mafunzo ya JKT kundi maalum la Jenga kesho iliyo bora (BBT) kikosi cha 834 Makutopola ikiwa ni oparesheni maalum ya miaka 60 ya Jeshi hilo.
“Mafunzo mliyo yapata hayakuwa mepesi hasa hapa JKT hivyo mnatikiwa kutoa heshima kwa kuhakikisha hazma ya serikali inafanikiwa kwa manufaa yenu na kwa taifa,”amesema Mhe. Bashe.
Amesema Rais Dkt. Samia yuko tayari kuendeleza juhudi za kuinua uchumi wa nchi hususani kupitia vijana na programu hiyo ya BBT ambapo pia amewasisitiza kudumisha ushirikiano baina yao na Wizara ya Kilimo.
Aidha Waziri Bashe amewahasa wananchi kuona fursa zilizopo kwenye kilimo kwani kimekuwa uti wa mgongo pamoja na kutoa rai kwa vijana kuchangamkia fursa pale wanapozipata na kuzitumia kutimiza malengo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa rai kwa taasisi zingine kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa watendaji wao kwani yanalenga kuwajengea vijana uzalendo kwa taifa lao, nidhamu nzuri, hali ya kufanya kazi bila kuchoka, umoja na mshikamano pamoja na uvumilivu wanapopambana na changamoto za kikazi na maisha.
“Ni imani yetu kuwa kila kijana aliyepata mafunzo haya anakuwa na mabadiriko chanya ya kiutendaji na uwajibikaji, vijana hawa wameapa mbele yako mgeni rasmi ambapo kihapo kile kinawaunganisha kwamba watakapo fanya kosa wanawajibika katika sheria zetu za kijeshi,”amesema.
Naye Kaimu kamanda kikosi 834 kikosi cha jeshi Meja James Macheta amesema kuwa mafunzo hayo waliyo yapata vijana yatawasidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kwa taifa.
Nao wahitimu wa mafunzo hayo wamesema wakati wakiwa katika mafunzo hayo wamejifunza masomo mbalimbali kwa nadharia na vitendo ambayo yamewafanya kuwa wazalendo, watii, wenye nidhamu, wachapakazi, wakakamavu na wenye fikra chanya ndani ya nchi.
Post a Comment
Post a Comment