Na John Walter-Manyara
Misaada mbalimbali kwaajili ya Waathirika wa Maafa Hanang yaendelea kutolewa.
Kampuni ya Vinywaji ya Bonite Bottlers Limited imewasilisha salamu zao za pole kwa waathirika wa Maafa ya Mafuriko Hanang kwakutoa mahitaji mbalimbali vikiwemo maji ya kunywa, Unga wa sembe, Mchele, Magodoro pamoja na vitu vingine vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 50
Aidha, Taasisi ya Arise and Shine chini ya Mchungaji Mwamposa wametoa misaada ya vitu mbalimbali vikiwemo Unga wa sembe, Magodoro kwa waathirika hao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akiambatana na viongozi wengine wameendelea kupokea misaada hiyo.
Post a Comment
Post a Comment