const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); AMO Foundation yawakumbuka waathirka wa Mafuriko Hanang' - HABARI MPYA

..

AMO Foundation yawakumbuka waathirka wa Mafuriko Hanang'


Na John Walter-Hanang'

Shirika lisilo la Kiserikali AMO FOUNDATION limetoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya udongo, tope, mawe na magogo yaliyotokea desemba 3, 2023 wilayani Hanang' mkoa wa Manyara.

Mwakilishi wa shirika hilo Ramadhani Rajabu amesema wamemuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa unga wa sembe tani 3, tani 1 ya Maharage na mafuta ya kula.

Rajabu amesema mkurugenzi wao Amina Said  ambaye yupo nje ya nchi  ameahidi atakaporeja nchini atawasili Katesh Desemba 27, 2023 kwa ajili ya kutoa misaada zaidi haswa vifaa vitakavyosaidia katika ujenzi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema msaada huo ni faraja kwa walioathirika na maafa hayo lakini pia kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha ameipongeza AMO FOUNDATION kwa kuguswa kwao kutoa misaada hiyo na kuahidi kuwa serikali inasimamia ipasavyo ili iwafikie walengwa.


Related Posts

Post a Comment