Na John Walter-Manyara
Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) mkoa wa Manyara kimeungana na watanzania wengine katika kuwafariji waathirika wa Maafa ya Maporomoko ya tope, mawe na magogo yaliyotokea desemba 3 mwaka huu wilayani Hanang'.
Chama hicho kimetoa msaada wa nguo na viatu kwa waathirika hao na kupokelewa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang' Francis Namaumbo.
Katibu wa CHANETA mkoa wa Manyara Lucy Sylvester pamoja wajumbe wa Chama hicho wamesema wamejichanga kama wana CHANETA na kutoa msaada huo ili wale wasio na nguo wala viatu waweze kujisitiri.
Post a Comment
Post a Comment