const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); RC Chalamila atoa maagizo manne kuukali mto Msimbazi - HABARI MPYA

..

RC Chalamila atoa maagizo manne kuukali mto Msimbazi


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila leo Januari 10, 2024 ametoa MAAGIZO MANNE (4) kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bonde la Wami/ Ruvu na Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam

Ameyatoa Maagizo hayo Manne (4) akiwa kwenye ziara yake aliyoifanya katika eneo la Vingunguti Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam alipofika kuangalia athari za mto Msimbazi kwa upana wake

RC Chalamila amezuia Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam kusafisha Mito na baadhi ya Maeneo yaliyomo humo badala yake zijikite kuwasimamia makandarasi wote ili Mito na Maeneo yaweze kuwa Safi


Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amewataka watu wa Bonde kutoa Vibali vya Dharura kwa watu wenye mitambo mikubwa  ( mashine ) na mshine
zenyewe zionekane ili kuweza kusafisha Mabonde na Mito hiyo na kuepuka janja janja za kukodisha mitambo

Hata hivyo RC Chalamila amewaagiza watu wa Bonde na kikosi kazi Cha  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusimamia vizuri upatikanaji wa michanga kwa Halmashauri zote zinapohitaji ili ziweze kuupata kwa urahisi na Bei nafuu

Mwisho kabisa RC Chalamila ameagiza kifanyike haraka Kikao Cha Usafi kitakachokuwa na Mkuu wa Wilaya, Watu wa Afya, Watendaji wa Mitaa ili kuzungumzia suala Hilo kwani Usafi kwa Utimilifu  kwani Usafi huo bado haujawa vizuri hivyo ameutaka kila mtaa ufike hatua ya  kujitambua na kufanya Usafi wenyewe

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogoro amekiri kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi

Related Posts

Post a Comment