Na, Mwandishi Wetu - DODOMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imepokea taarifa ya Programu ya kukuza Ujuzi wa Nguvu Kazi nchini inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizungumza Januari 24, 2024 baada ya kupitia na kuchambua wasilisho la Ofisi hiyo Fungu 65 kuhusu programu hiyo, amesema wasilisho hilo litasaidia kamati kutoa ushauri utakaoongeza ufanisi kwenye utekelezaji wake wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema serikali imeendelea kutanua wigo wa ukuzaji ujuzi kwa vijana na hadi sasa wamenufaika 141,968 kupitia programu ya kukuza ujuzi iliyoanza kutekelezwa Mwaka 2016/17.
Post a Comment
Post a Comment