Rais wa wamu ya tatu, Mzee Benjamin Makapa atakumbukwa sana na wapinzani kufuatia kauli yake aliyoitoa mwaka 2015 wakati wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mkuu za CCM ambapo alisema kuwa, wanaosema wanataka kuikomboa nchi ni Wapumbavu na Malofa.
Mzee Mkapa aliyesema hayo katika uwanja wa Jangwani Jijini Dar es Salaam wakati chama chake kikizindua kampeni za uchaguzi wakati akimnadi mgombea aliyepitishwa, John Pombe Magufuli.
Licha ya kuwa Mzee Mkapa hawakuwataja moja kwa moja aliowaita wapumbavu na malofa, lakini ni dhahiri kuwa maneno hayo yaliwahusu wananchama wa vyama vya upinzani waliokuwa wakisema kuwa wanataka kuiomboa nchini kutoka mikononi mwa CCM. Mzee Mkapa alisema hao ni wapumbavu na malofa kwani nchi tayari ilishakombolewa tangu mwaka 1961.
Akizungumza leo katika hafla ya kuzindua nyumba 50 za watumishi wa afya katika mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera, Mzee Mkapa ameyakumbushia maneno hayo na kusema maendeleo haya yatawasaidia sana wale aliowaita hivyo.
Wale niliowaita wapumbavu na malofa, naamini maendeleo haya katika sekta ya afya yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa upumbavu wao, alisema Mzee Mkapa huku umati wa watu waliohudhuria wakicheka.
Kabla Mkapa hajazungumza, Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Kasheku Musukuma alisema kuwa, watu hawahitaji tena tafsiri ya hayo maneno yaliyotolewa mwaka 2015, kwani kufuatia jitihada za dhati za kuleta maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli, watanzania sasa wanajua wapumbavu na malofa ni akina nani.
Nyumba hizo ambazo Mzee Mkapa amekabidhi leo zimejengwa na Mkapa Foundation ambapo, tangu taasisi hiyo imeanza kufanyakazi, tayari imejengwa nyumba 450 katika mikoa 17 nchini huku ikiwa imewasomesha madaktari zaidi ya 960.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli alimpongeza Mzee Mkapa kwa jitihada zake na kusema kuwa, angeweza kukaa nyumbani na kufaidi mafao yake baada ya kumaliza urais, lakini amemaua kuendelea kuwatumikia watanzania.
Post a Comment
Post a Comment