Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Mji ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui ya uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo.
Uzinduzi huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika ukumbi wa Desire Park .
Akizungumza juu ya hatua ya kukwama kwa uzinduzi huo Naibu Waziri Wambura, amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo Bi, Rosemery Michael, amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa husika.
Baadhi ya wasanii na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu Hiyo, Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo kutokuzinduliwa.
Manase Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi ambaye anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) amefafanua kuwa wao hawana ugomvi na sanaa wala na wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.
Post a Comment
Post a Comment