Wakati Tamasha la Fiesta katika mkoa wa Dar es Salaam likiendelea usiku wa kuamkia leo, Rais wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania, John Magufuli aliwapigia simu waandaaji wa Tamasha hilo Clouds Media na kuwaambia kwamba waongeze muda wa kumaliza tamasha hilo hadi saa 12 alfajiri.
Rais Magufuli alipiga simu hiyo na kusema tamasha hilo lifanyike mpaka saa 12 kamili asubuhi ambapo hapa chini ni nukuu ya kilichoandikwa kwenye ukurasa wa CloudsFM katika Mtandao wa Instagram.
“Tumepokea simu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema #TigoFiestaKubwaLao iende hadi saa 12 asubuhi. Yani akienda Kanisani anapishana na watu wanatoka Fiesta”
“Sisi tunashukuru sana, Asante sana Rais wetu kwa kuonyesha upendo kwa kiwanda cha burudani, tutaendelea kusimamia tasnia hii kwa maslahi ya Taifa letu #BabaKasema #JPMnaMuziki“ wameandika Clouds Media.
Post a Comment
Post a Comment