Kuna tetesi kwamba WhatsApp ipo mbioni kurudisha status za maneno baada kuondoa huduma hiyo katika toleo lake la hivi karibuni, hii ni habari nzuri kwa watumiaji ambao hawakupendezwa na mfumo mpya ulioletwa mwezi uliopita.
Muonekano mpya wa WhatsApp baada ya mabadiliko ya status
Kulikuwa na maneno mengi baada ya WhatsApp kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa status kwa kutambulisha namna ya kuweka status inayofanana na mfumo unaotumiwa na mtandao wa Snapchat, baadhi waliufurahia utaratibu huu lakini kulikuwa na wengi ambao waliona mabadiliko haya kama kosa kubwa kutoka kwa WhatsApp.
Nini chanzo cha tetesi hizi!?
Tetesi za kurudishwa kwa huduma ya status za maneno katika WhatsApp zinakuja baada ya toleo la WhatsApp beta kuletwa likiwa sio tu na mfumo mpya wa status lakini pia mfumo wa status za maneno kama zamani. Hata hivyo bado watumiaji watalazimika kutumia app hii pendwa pamoja na vipengere vipya ambavyo vililetwa na mwezi uliopita.
Nini Kingine kipya kipo jikoni?
Kunatetesi kwamba Whatsapp pia ipo mbioni kuyaruhusu makampuni kuweza kuwatumia taarifa mbalimbali watumiaji wa mtandao huu, taarifa hizi zinahisiwa zitakuwa ni aina fulani ya matangazo ama taarifa kuhusu huduma fulani. Ingawa hatua hii inaweza kupata upinzani mkubwa kutoka kwa watumiaji lakini msukumo wa wawekezaji ni dhahiri ndio utakaokuwa uamuzi wa mwisho.
Mabadiliko haya yatawafikia wakina nani?!
Ingawa sio kila kinachojaribiwa katika WhatsApp beta hufanikiwa kuingia katika soko lakini kuna nafasi kubwa huduma hizi zinazojadiliwa zikawafikia watumiaji wa kawaida siku za usoni.
Post a Comment
Post a Comment