Nokia wanarudi kivingine!!
By Ibrahim,(@rackeetz)
Hii ni kwa wapenzi na mashabiki wa Nokia ambao wana hamu ya 'kupyatila' vidole vyao kwenye simu mpya ya Nokia.Habari njema ni kuwa hivi sasa zile kero za mifumo ya Microsoft hazitakuwemo katika simu hii mpya.
Unataka kuwa wa kwanza kuipata simu hii mpya??
Twendzetu kwa akina Xi Jin Ping... China ili tuweze kununua simu hii mpya ya NOKIA inayotumia mfumo wa ANDROID(Android-powered Nokia) kutoka kwa kampuni yenye makao yake makuu nchini FINLAND ambayo ndo imehusika katika utengenezaji wa simu hii.
Kampuni hiyo inafahamika kama HMD, ilianzishwa mwaka jana na kundi la 'Wana-Nokia' wa zamani.. yaani wafanyakazi wa Nokia wa zamani, wakiwa na lengo la kutengeneza muundo mpya wa Nokia kwa leseni na vibali halali kutoka kwa mmiliki wa Nokia, Microsoft.
HMD ilitoa simu mbili mwezi uliopita kwaajili ya maonesho.Hatimaye wametangaza uzinduzi rasmi wa simu hii mpya, ya kisasa zaidi.. wenyewe wanaiita NOKIA 6.Inatarajiwa kuzinduliwa nchini China mapema mwaka huu.
Utahitaji kununua mtandaoni? Usije sema sikukwambia.. msambazaji alieidhinishwa ni JD.com kwa mtonyo wa $245 sawa na Tshs 547,575/=.
Twende taratibu... Tshs 547,575/=? Hiyo simu ina kipi labda?
~Imetengenezwa kwa aluminum iliyong'arishwa kwa kiwango cha juu
~Kioo aina ya Gorilla chenye upana wa 5.5 inch kinachoonyesha picha na maandishi kwa ubora wa hali ya juu(HD screen) ambapo kwa haraka haraka, ni zaidi ya iPhone.
~Ina processor aina ya Qualcomm Snapdragon 430
~Ina RAM 4GB, 64GB storage
~Inatumia mfumo wa kisasa kabisa wa Android duniani kwa sasa(Nougat OS).
~Ina spika mbili za nje (Dolby Atmos audio),
~Kamera ya kawaida 16MP na ya mbele 8MP (zote ni f/2.0).
Akiongelea uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji,anayeitwa Arto Nummela, alitaja sababu kadhaa zinayoifanya NOKIA 6 kuwa bora zaidi kuwa ni UIMARA,MUUNDO WAKE pamoja na VITU VINGI VINGINE vilivyowekwa ili kuhakikisha unapata burudani na muonekano mzuri.Nanukuu “Nokia 6 ni matokeo ya kuwasikiliza wateja wetu ambao wanastahili kifaa kizuri chenye uimara wa kila namna,burudani na muonekano nadhifu" alisema.
Sasa, kwanini HMD wamelenga soko la China?
Tunarudi kwenye ukubwa wa soko la 'simu janja'(smartphone) duniani... China ilikuwa na watumiaji zaidi ya milioni 552 mwaka uliopita.Matarajio ni kuwa watumiaji wataongezeka kufikia zaidi ya Milioni 593 mwaka 2017 — kimkakati ni muhimu sana(“strategically important”).Hivyo hii ni mbinu ya kutafuta mauzo makubwa katika soko linalokua kwa kasi, bila si lingine bali CHINA.
Nummela ameongeza kuwa kampuni yake ya HMD itaongeza utengenezaji wa simu na kuzisambaza duniani kote miezi kadhaa ijayo,ikionekana kama mkakati wa kuimarisha mauzo.
Mimi.. ninashukuru.
Source:Techcrunch
#rackee

Post a Comment
Post a Comment