const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Fedha nyingi za miradi zimekuwa kikipotea kwa sababu ya Rushwa - HABARI MPYA

..

Fedha nyingi za miradi zimekuwa kikipotea kwa sababu ya Rushwa

Post a Comment


Charles Nakembetwa, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe
SERIKALI mkoani Njombe imesema kuwa imekuwa ikipoteza fedha nyingi pamoja na kusababisha huduma mbovu kwa wananchi kutokana na vitendo vya rushwa vinavyofanywa na viongozi na watendaji wa serikali. 

Kauli hiyo inatolewana kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Charles Nakembetwa wakati akizungumza na madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Akiwa katika baraza la madiwani Nakembetwa anasema kuwa fedha nyingi zimekuwa zikiishia makonono mwa watu wabaya badala ya kukamilika miradi na jamii kukosa huduma bora.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Valentino Hongoli anasema kuwa anaomba takukuru kupunguza mirorongo baada ya watu kutoa taarifa za ubadhilifu. 
Hata hivyo mkuu wa wilaya anasema kuwa kwa mtumishi yeyote atakaye tajwa kwa vitendo vya rushwa ni lazima ashikiliwe kwanza.

Katika maeneo mbalimbali ya miradi ya jamii hasa ile mikubwa inayo gharimu mamilioni ya fedha kumedaiwa kutolewa kwa rushwa na kuifanya miradi hiyo kujengwa kwa thamani ndogo tofauti na ilivyo tarajiwa huku watendaji wakigawana pesa,
ANGALIA VIDEO CHIDEO

Related Posts

Post a Comment