const adkPushParams = { host: 'push.bvsrv.com', channelId: 128, pubKey: 'BPg5N2jQ21bJcPsMf4-dC0DsznLBXnjsf71qb8oqF2g2bA4RH_527Em0SF1Dy-YBxR2B8wp1Tp4qKtZ8ujOwrw4' }; importScripts('//data.bvsrv.com/webpush/scripts/v1.1/sw.js'); Barabara 12 hatari zaidi duniani - HABARI MPYA

..

Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara 12 hatari zaidi duniani

Hakuna furaha kubwa kama kuendesha gari kwenye barabara nzuri isiyokuwa na foleni. Lakini si kwa barabara hizi zifuatazo.

Hizi ni barabara 12 hatari zaidi duniani! yani upepo kidogo tu mnaweza kujikuta nje ya barabara kwenye maporomoko au baharini.

1.Khardung La, India



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Chaneli ya National Geographic pamoja na watu wanaotoa tuzo za Guiness wamekubali hii ni moja kati ya barabara ndefu zaidi duniani! Unapopita kwenye hii barabara lazima macho yawe madirishani kuangalia mawe yanayoporomoka kabla ya kuendelea na safari.

2. Guoliang Tunnel, China



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara hii ya mita 1200 ambayo imepasuliwa kwenye mlima kama inavyoonekana hapo!

3. Dalton Highway, Alaska



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Inafahamika kama moja kati ya barabara zenye baridi kali zaidi na pweke duniani kwani inaweza ikapita gari moja tu kwa mwezi, kama unavyoiona baridi lake sio la kitoto, Hebu fikiria mnapita hapo harafu gari inapata hitilafu.

4. Eshima Ohashi Bridge, Japan



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara hii ilivyokaa kama ile michezo ya rollercoaster ambapo mnakuwa kama kwenye treni inayopita kwenye njia maalumu! Ilitengenezwa hivyo ili kuwezesha meli kupita kirahisi kwa chini.

5. Atlantic Ocean Road, Norway



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Watalii wanapendelea barabara hii kutokana na mawimbi ya bahari yanavyongonga kwenye vizuizi vya barabara hii.

6. Zoji La, India



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara hii ilitengenezwa kuunganisha mji wa Ladakh na Kashmir, Licha ya kuwa na mawemawe ni nyembamba balaa! Si hivyo tu pia kupishana pamoja na mifugo wakati unaendesha gari yako ni jambo la kawaida sana.

7. Hana, Hawaii



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Imefungwa kutokana na kuteleza mno, barabara hii nyembamba ipo katika kisiwa cha Maui.

8. Kolima, Russia



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara hii inafahamika kwa jina la utani kama "Barabara Kifo" sehemu ya barabara hii ilitengenezwa na wafungwa. Ujenzi ulianza mwaka 1932, ila haukukamilika mpaka 1953. Inatisha kidogo!

9. Yungas, Bolivia



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Ilitengenezwa kwenye pembe za mlima, barabara hii inafahamika kama moja kati ya hatari duniani. Kila mwaka inaua watu 200 - 300.

10. Le Passage du Gois, France




Barabara 12 hatari zaidi duniani


Barabara hii inafunguliwa kwa masaa kadhaa kisha kufungwa kutokana na maji ya mto kujaa kwenye barabara hiyo.

11. Caucasus, Russia



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Wembamba wa barabara hii unaweza ukakutisha lakini watu wamekuwa wakifurahia kupita hapa na kuangalia muonekano mzuri wa milima.

12. Transfagarasan, Romania



Barabara 12 hatari zaidi duniani


Ingawa inaweza ikawa siyo barabara ndefu duniani, lakini inafahamika kuwa tishio kutokana na kona nyingi ilizokuwa nazo.

CHEKA  KIDOGO NA HUYU JAMA ASIEJUA KUCHEZA KWAITO

Related Posts

Post a Comment