Mamia ya wafanyakazi huenda wakakosa ajira Afrika Mashariki baada ya maduka ya jumla ya Nakumatt kuonekana kuwa hatarini.
Nakumatt iliyo na maduka nchini Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda inakabiliwa na changamoto za kulipa madeni yake, na sasa wadeni wake wanatishia kuweka mali ya Nakumatt kwenye mnada.
Kwa miaka kadhaa Nakumatt imejivunia kukidhi mahitaji yote ya wateja na kauli mbiu ya 'You need it, we've got it' (Unahitaji, Tunacho), lakini hivi karibuni hata bidhaa muhimu kama mkate zimekuwa nadra kupatikana kwenye rafu zake.
Wateja wa duka hilo la Jumla walitaka kutambua yanayojiri kwenye duka hilo kupitia mtandao baada ya kukosa bidhaa muhimu lakini wasimamizi wa maduka hayo wamekanusha madai kwamba huenda biashara yake ikaporomoka.
Pindu tu baada ya habari kuanza kuenea mitandaoni, ilianza kubainika wazi kuwa maduka hilo haliwezi tena kuwalipa wanaoyauzia bidhaa.
Nakumatt pia inadaiwa kushindwa kulipa kodi ya majumba ambayo yanatumiwa kwa maduka yake.
Wiki moja tu baada ya kufunga maduka matatu nchini Uganda, madalali wametwaa mali ya Nakumatt kwenye jumba moja la kibiashara viunganimwa jiji la Nairobi, kwa madai ya kutolipwa kodi ya takriban dola nusu milioni.
Aidha kampuni hiyo inakabiliwa na kesi nyingine ya kufilisika kwa kutolipa deni la zaidi ya dola laki saba, na kwa kuandika cheki hewa.
Serikali ya Kenya imeingilia kati majadiliano baina ya duka hilo na wadeni wake, ili kupata suluhisho litakalozuia kampuni hiyo kusambaratika, haswa kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya mwezi Agosti.
Post a Comment
Post a Comment